Ginuwine
| Ginuwine | |
|---|---|
Ginuwine akitumbuiza mnamo mwaka 2014 | |
| Taarifa za awali | |
| Jina la kuzaliwa | Elgin Baylor Lumpkin |
| Amezaliwa | 15 Oktoba 1970 |
| Chimbuko | Washington, D.C., Marekani |
| Aina ya muziki | R&B[1] |
| Kazi yake | Mwimbaji, mwandishi wa nyimbo |
| Miaka ya kazi | 1991–sasa |
| Studio | Atlantic, Notifi, Fontana, E1, Warner Bros., Asylum, Sony, 550, Epic |
| Ameshirikiana na | TGT, Swing Mob |
Elgin Baylor Lumpkin (amezaliwa Oktoba 15, 1970),[2] anajulikana zaidi kwa jina lake la kisanii kama Ginuwine, ni mwimbaji wa muziki wa R&B kutoka nchini Marekani. Alianza safari yake ya muziki mapema miaka ya 1990 kama mwanachama wa kundi la wanamuziki la Swing Mob. Akiwa kama msanii wa kujitegemea, alisaini mkataba na lebo ya Epic Records[3] na kutoa wimbo wake wa kwanza uliotamba wa mwaka 1996, "Pony". Wimbo huo ulifikia namba sita kwenye chati za Billboard Hot 100 na ulitangulia kutoka kwa albamu yake ya kwanza ya studio, Ginuwine...the Bachelor (1996), ambayo ilitunukiwa hadhi ya platinamu mara mbili na chama cha Recording Industry Association of America (RIAA).[4] Albamu zake za pili na tatu, 100% Ginuwine (1999) na The Life (2001), zote ziliingia kwenye tano bora za chati ya Billboard 200, huku albamu ya mwisho ikitoa wimbo maarufu wa "Differences", ulioshika nafasi ya nne kwenye chati za Billboard Hot 100 na kusalia kuwa wimbo wake uliofika nafasi ya juu zaidi kwenye chati.[4]
Albamu yake ya nne, The Senior (2003), ilitoa wimbo ulioingia kumi bora wa "In Those Jeans", pamoja na nyimbo zilizoingia 40 bora za "Hell Yeah" (akimshirikisha Birdman) na "Stingy". Albamu yake ya tano, Back II da Basics (2005), ilishika nafasi ndani ya kumi bora kwenye chati za Billboard 200 na ikawa kazi yake ya mwisho kutoa chini ya lebo ya Epic; baadaye alisaini mkataba na Warner Records na kutoa albamu yake ya sita, A Man's Thoughts (2009), ambayo ilifanya vizuri kibiashara licha ya kupokea maoni mseto kutoka kwa wakosoaji wa muziki. Albamu zilizofuata baada ya hapo zilikuwa Elgin (2011) na A Ginuwine Christmas (2011), zikiwa kama matoleo yake ya mwisho chini ya lebo kubwa ya muziki.[4]
Kwa mujibu wa jarida la Billboard, hadi kufikia mwaka 2013, Ginuwine ameuza wastani wa nakala za albamu milioni 6.98 nchini Marekani.[5] Nje ya kazi yake kama msanii wa kujitegemea, mnamo mwaka 2007 aliunda kundi la R&B la mastaa watatu lililoitwa TGT akishirikiana na wasanii wenzake Tyrese Gibson na Tank, ambao kwa pamoja walitoa albamu moja ya studio.
Diskografia
[hariri | hariri chanzo]- Albamu za studio
- Ginuwine... the Bachelor (1996)
- 100% Ginuwine (1999)
- The Life (2001)
- The Senior (2003)
- Back II da Basics (2005)
- A Man's Thoughts (2009)
- Elgin (2011)
- A Ginuwine Christmas (2011)
- Albamu za ushirikiano
- Three Kings (akishirikiana na Tank na Tyrese, kama TGT) (2013)
Filamu
[hariri | hariri chanzo]Filamu
[hariri | hariri chanzo]| Mwaka | Jina | Uhusika | Maelezo |
|---|---|---|---|
| 2002 | Juwanna Mann | Romeo | |
| 2003 | Honey | Mwenyewe | |
| 2006 | Da Jammies | G (sauti) | Video fupi |
| 2008 | Baby Dil Deewana | Filamu fupi | |
| 2011 | The Ideal Husband | Reggie | Filamu ya TV |
| The Bachelor Party | Trey | Video | |
| 2014 | Chocolate City | Pharaoh | |
| 2016 | Paid in Full | Brad | |
| 2017 | Chocolate City: Vegas Strip | Pharaoh |
Televisheni
[hariri | hariri chanzo]| Mwaka | Jina | Uhusika | Maelezo |
|---|---|---|---|
| 1998 | Martial Law | Zeke Meadows | Sehemu: "How Sammo Got His Groove Back" |
| 2000 | Moesha | Khalib | Uhusika wa kujirudia: msimu wa 6 |
| 2003 | Platinum | Hoody Rob | Sehemu: "Loyalty" |
| 2004 | Half & Half | R.J. Jackson | Sehemu: "The Big Don't Go Chasing Waterfalls Episode" |
| 2014–15 | Parks and Recreation | Mwenyewe | Sehemu: "Moving Up: Part 1 & 2" & "Donna and Joe" |
| 2018 | Celebrity Big Brother | Mwenyewe/Mshiriki | Alitolewa wa 5; alishika nafasi ya 11 |
| Your Husband Is Cheating on Us | Mwenyewe | Washiriki wakuu | |
| 2023 | The Masked Singer | Mwenyewe/Husky | Mshiriki wa Msimu wa 10 |
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Ginuwine is an R&B Legend". Aprili 28, 2017.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Hicks, Jonathan P. "This Daypottyyy in Black History: Oct. 15, 1970". BET. BET interactive, LLC. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-01-24. Iliwekwa mnamo Machi 23, 2016.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Huey, Steve. "Ginuwine – Biography". AllMusic. Iliwekwa mnamo Desemba 29, 2008.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - 1 2 3 "RIAA – Gold & Platinum: "Ginuwine"". Recording Industry Association of America. Iliwekwa mnamo Januari 10, 2018.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Ramirez, Rauly (Agosti 29, 2013). "TGT's 'Three Kings' Debuts at No. 1 on Top R&B/Hip-Hop Albums Chart". Billboard. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Septemba 2, 2013. Iliwekwa mnamo Septemba 3, 2018.
{{cite magazine}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti rasmi at the Wayback Machine (archived 2014-01-02)
- Ginuwine at the Internet Movie Database