Audrey Hepburn
Mandhari

Audrey Kathleen Hepburn-Ruston (née Ruston; 4 Mei 1929 – 20 Januari 1993)[1] alikuwa mwigizaji na mwanaharakati wa kibinadamu wa Uingereza. Akitambuliwa kama nembo (icon) ya filamu na mitindo, aliorodheshwa na Taasisi ya Filamu ya Marekani (American Film Institute) kama mwigizaji wa kike wa tatu kwa ubora katika historia ya sinema ya zamani ya Hollywood (Classical Hollywood cinema).[2][3]
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Audrey Kathleen Ruston (baadaye, Hepburn-Ruston) alizaliwa katika nyumba namba 48 kwenye Barabara ya Keyenveld huko Ixelles, Brussels, Ubelgiji. Alijulikana kwa familia yake kama Adriaantje. Alilelewa katika misingi ya Kiprotestanti na alidumu katika imani hiyo maisha yake yote.[4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://web.archive.org/web/20221005150312/https://www.history.com/this-day-in-history/actress-audrey-hepburn-dies
- ↑ https://www.imdb.com/name/nm0000030/bio/
- ↑ https://www.biography.com/actors/audrey-hepburn
- ↑ https://www.openculture.com/2015/08/audrey-hepburns-moving-screen-test-for-roman-holiday-1953.html
| Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Audrey Hepburn kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |